Mstahamilivu hula mbivu, mtaka cha uvunguni sharti ainame, na mchumia juani hulia kivulini. Ni machache ya maadili yamuongozayo binti Malaika katika safari yake ya kutimiza ndoto zake. Kujiendeleza kielimu ndiyo ndoto yake kuu. Kwa vile Mungu hamtupi mja wake, anabahatika kwenda ughaibuni kitaaluma. Ni safari inayomtenganisha na mpenzi wake, Ben. Lakini Ben anaahidi kumsubiri hadi afuzu masomo yake. Katika kipindi hiki cha utengano, dunia inawapangia...