Pela anawapenda wanyama. Siku moja mvua kubwa inanyesha na kuangusha mti mkubwa nje ya nyumba yao. Asubuhi Pela anatengeneza nyumba kutokana na matawi na majani ya mti huu na kuwaalika marafiki wake - Ndege, Kuku, Paka na Mbwa. Asichokijua ni kuwa hawa marafiki hawawezi kukaa pamoja, jambo linalomhuzunisha sana.