Maelezo ya Kitabu
Chuaro alilelewa katika eneo la mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini. Kwa masomo yake ya shule ya upili, alihudhuria shule ya bweni katika kijji cha Transkei ambapo watu waliishi maisha ya kizamani. Yeye na marafiki zake walifikiri wasichana katika maeneo hayo ya mashambani walikuwa wajinga kwa sababu hawakuvaa kama wao na walisumbuka zaidi kwamba wasichana hawakufunika matiti yao. Jumamosi moja alasiri walipokuwa wakitembea, walikutana na wasichana wa mashambani na kuwauliza kwa nini hawakuvaa sidiria au blauzi. Wakati huohuo, wasichana wa jiji walijifunza kwa njia ngumu kwamba hawa wasichana wa vijijini walikuwa na akili sana, na kuwafanya watilie shaka akili zao wenyewe.