Uongozi mzuri hutendea watu haki. MFUTA KAULI-kiongozi mkuu wa nchi ya Ukiwa ambaye hujinasibu kuwapenda watu anaowaongoza, tena husema mara kwa mara kuwa anawatendea haki. Mara kadhaa ameshirikiana na wawekezaji wezi kuwanyang'anya mashamba yao. Wananchi Wengi wa nchi ya Ukiwa ni watu wasio na elimu- ni watu wenye Ukiwa wa elimu na ufahamu. Katikati ya hayo yote anaibuka kijana aitwaye KIRAKA, anadhamiria kuikomboa jamii hii kutoka kwenye unyanyasaji wa MFUTA KAULI. Ujasiri wake katika kuziba matundu ya unyanyasaji na uonevu katika jamii ya nchi ya Ukiwa unaonyesha maana halisi ya jina lake.Kwa kufanya hivyo anajikuta ametangaza vita dhidi ya MFUTA KAULI. Maisha ya Kiraka yanabadilika na kuwa machungu, kila siku anawindwa na askari wa MFUTA KAULI. Watu wachache wanamuita mkombozi ila wengi wanamuona kuwa ni mtu hatari kwa usalama wa nchi ya Ukiwa. Hakati tamaa, anasonga mbele kwa ujasiri mkubwa. WASIFU WA MWANDISHI. MNIKO CHACHA ni mwandishi wa vitabu Vitano ambavyo ni;- Songs of African Fathers, Storms and Pleasures, Kiraka Cha Ukombozi, Weka Pesa Pata Pesa, na An Enemy of the Villagers. Mwaka huu, 2022 atachapisha riwaya mpya itakayojulikana kwa jina la 'Nitalipa Mahari na kuoa.'
ThriftBooks sells millions of used books at the lowest everyday prices. We personally assess every book's quality and offer rare, out-of-print treasures. We deliver the joy of reading in recyclable packaging with free standard shipping on US orders over $15. ThriftBooks.com. Read more. Spend less.